Na , Murtadhwa Elbahsan, simanjiro
Arusha. Wananchi wa jamii ya wafugaji wanaoishi katika kata
ya Naisinyai wilaya ya Simanjiro inayopakana na machimbo ya Tanzanite
wameshauriwa kuanza kujikita katika ujasiriamali badala ya kutegemea
mifugo pekee.
Mkurugenzi mwenza wa kampuni Tanzanite One,Faisal Juma
alitoa wito huo jana wakati akitoa msaada wa sh 15 million kwa wanawake
wa Kata hiyo ili kuanzisha chama cha kuweka na kukopa(SACCOs).
Juma alisema, wananchi wa Naisinyai wamepata fursa ya kuwa
katika eneo ambalo yanachimbwa madini ya Tanzanite hivyo ni muhimu
wanufaike nayo kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na
kufanyabiashara ,kuchimba na kuuza madini hayo.
"Sisi kama Tanzanite One tunawajibu kuwasaidia kuwa
wajasiriamali kwani tunachimba madini katika kata yenu na huu ni msaada
kwa wajasiriamali lakini bado tutaendelea kusomesha watoto wa Kaya
masikini na kutoa Michango mingine" alisema
Alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sana mifugo
hivyo ili kutoathiri maisha ya wafugaji wanapaswa kuwa na mbadala wa
kidogo wa kuwasaidia kimaisha.
Awali mwenyekiti wa kijiji cha Naisinyai,Taiko Laizer
alishukuru michango wawekezaji na kuwataka kupanua wigo wa kutoa ajira
kwa wananchi wa Naisinyai hasa wanawake.
''Tunajua mmewapa ajira vijana wa hapa lakini tunaomba zinapotokea ajira hasa wanawake tuongezewe" alisema
Naye Diwani wa viti maalum Kata ya Naisinyai Paulina Masekeni aliahidi fedha waliopatiwa, Wanawake wa kata hiyo zitatumika kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kama walivyo omba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni